MAKALA YA UCHUMI: VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUJIKWAMUA KIUCHUMI Posted on 04:45 by PRINCE MEDIA TZ with No comments Na Ferdinand Shayo,Arusha. Licha ya fursa lukuki za kiuchumi zilizoko nchini bado vijana wengi hawana ajira bado vijana wengi ni masikini hali inayoshangaza na kusikitisha pia. Hulka ya vijana kuwa watu wa kulalamika imepofusha macho ya ndani na ya nje ya kuona fursa zilizopo kwenye mazingira yao kuzitumia kujiingizia kipato na kubadilisha maisha yao. Vijana wengi hata wasomi wamekua wakiwalalamikia serikali,mazingira,jamii hali ambayo imetengeneza ukuta kati yao na fursa kiasi cha kutoziona wala kunufaika nazo. Katika dunia tunayoishi watu wachache sana ni matajiri na wengi ni masikini kwasababu matajiri wamejifunza kuyafanyia kazi malalamiko na matatizo ya watu kuyatafutia ufumbuzi na kuyatumia kama fursa ya kufanya biashara na kufanikiwa. Matatizo ya afya,chakula,usafiri,miundombinu,magonjwa,kukosekana kwa maji safi ya kunywa ,matatizo haya tayari kwao ni mtaji mkubwa ambao wakiyatafutia ufumbuzi . Wakati watu wengi wanajiuliza maswali ya mambo fulani na kukazana kuulizana wao huenda mbele zaidi na kutafuta majibu ya maswali ya jamii. “Asilimia 2% ya watu duniani ni matajiri wameamua kujitoa kwenye kundi la watu wanaolalamika na kutafuta suluhu ama ufumbuzi wa masuala mbali mbali ,asilimia 98% ni masikini ambao ni wengi hawa ni walalamikaji” Anaeleza Mjasiriamali Mashuhuri Erick Shigongo katika ukurasa wake wa facebook Ili kupiga hatua kuondokana na umasikini na tatizo la ukosefu wa ajira ni lazima kutoka kwenye kundi la walalamikaji na kuingia kwenye kundi la asilimia 2 ambao ni matajiri kwa kuamua kutafuta suluhu ya matatizo ya jamii na kuigeuza kuwa fursa ya kibiashara itakayobadilisha maisha yako. Ni vyema kuwa mtanguliaji wakati wengine wanawaza matatizo,changamoto nenda mbali zaidi fikiria kuja na suluhisho la matatizo yako kwa kufanya hivyo utakua umeisaidia jamii,familia,taifa na dunia huku ukijipatia kipato. Viko vikwazo mbali mbali vinavyomkwamisha kijana wa kitanzania kutumia fursa kubadilisha maisha yao mojawapo ni kutokufanya utafiti wa kina kujua jamii inahitaji nini? na imepungukiwa na nini? Ukosefu wa mitaji ni tatizo kubwa kwa vijana wengi hasa wale ambao tayari wameziona fursa wanataka kuzitumia kubadilisha maisha yao wanakwamishwa na mitaji. Mifumo isiyorafiki ya taasisi za fedha kwa vijana yenye masharti magumu ,riba kubwa hasa vijana wanaohitimu katika vyuo vikuu wanapokumbana na sharti la kuwa na ardhi,nyumba na mali zisizohamishika ili waweze kukopesheka wanavunjika moyo. Familia,jamii,serikali na taasisi binafsi ziungane kuwawezesha vijana kutumia fursa zinazowazunguka kubadilisha maisha yao ,ya familia zao,jamii,taifa na dunia. Tubadili mitazamo ya kuwaona ni sehemu ya matatizo katika jamii bali tuwaone kama ni sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyopo kwenye jamii kwasababu vijana wana nguvu,vipaji,uwezo wa ajabu,ubunifu . Nguvu za vijana zikitumika vizuri zinaweza kufukuzisha umasikini,utegemezi na matatizo lukuki yanayoikumba jamii. Vijana nao wasikae nyuma katika masuala ya kifamilia ,kijamii,wawajibike watumie nguvu walizonazo,ubunifu,uwezo,vipaji na talanta na elimu walizonazo katika kutatua changamoto za jamii badala ya kukaa kama watu wa pembezoni. Ni vyema kuhamasisha ushiriki mpana wa vijana katika masuala ya kiuchumi,kijamii na kisiasa kwasababu vijana wakiachwa nyuma hali itazidi kuwa mbaya kwa vizazi vijavyo. “Nusu ya maisha tunayoishi yanatokana na kizazi kilichopita na nusu nyingine inatokana na kizazi kilichopo” Anaeleza Mtunzi mmoja wa kitabu Ina maana kuwa vijana wanawajibika kuweka misingi bora ya kiuchumi,kimaadili na kiuwajibika misingi ambayo itatumiwa na kizazi kijacho iwapo hawatafanya hivyo hali itazidi kuwa mbaya . “Unapoacha kutimiza wajibu wako duniani,kutumia uwezo ulionao,vipaji unapokufa unaacha nafasi wazi duniani ambayo ingepaswa uijaze kwa kuacha kitu duniani kizazi kijacho kikija kitakuta nafasi uliyoiacha hukufanya kitu” Anaeleza Mtunzi Mashuri wa vitabu Myles Munroe. ferdinandshayo@gmail.com 0765938008 Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
0 comments:
Post a Comment