Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai akiwaasa watoto wa kike kuzingatia elimu kwani ndio nguzo ya
msingi katika maisha yao wakati w siku ya Mtoto wa Kike Duniani
iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Tandale jijini Dar. (Picha na
Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
Na Mwandishi wetu
WAKATI
serikali imekiri kwamba pamoja na kuwa na sheria kali za kuzuia ukatili
kwa watoto bado kuna matukio mengi yanayowanyima watoto uhuru na haki
zao msingi,wadau mbalimbali walioshiriki tamasha la mtoto msichana
wamewataka wasichana kutimiza ndoto zao.
Katika
tamasha hilo lililofanyika katika shule ya msingi Tandale, wilaya ya
Kinondoni mkoani Dar es salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane
vipaji mbalimbali vya watoto vilioneshwa na watoto nao kutoa kauli zao
za kutaka haki na ustawi wao kwani wao ni taifa la sasa.
Pamoja
na watoto hao kutoa ushuhuda na kuonesha njia ya kusaidiwa, Mkurugenzi
wa watoto kutoka wizara ya maendeleo ya jamii , jinsia na watoto
Margaret Sawe Mussai pamoja na kuwaambia watoto na jamii kutumia simu
119 kuelezea ukatili, ametaka madawati yaliyopo Polisi kutumika vilivyo
kukabiliana na vitendo hivyo.
Alisema lazima wazazi na walezi wawajibike katika kulinda watoto kwani taarifa zilizopo sasa haziridhishi hata kidogo.
Alisema
taarifa zilizopo watoto wa kike asilimia 29 na wavulana asilimia 13
wamenyanyaswa kijinsia wakati wasichana asilimia 14 na wavulana asilimia
6 wamekabiliwa na tatizo la kujaribiwa kuvurugwa kijinsia.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar.
Akizungumzia
suala la mimba za utotoni alisema kwamba wizara imeandaa program za
kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni huku akisema kwamba sheria ya
ndoa ya mwaka 1971 iko mbioni kubadilishwa ili kupandisha umri wa
kuolewa kuwa miaka 18.
Aidha
alisema serikali na wadau wengine wanaendesha mafunzo ya kuwatoa watoto
katika mazingira hatarishi pamoja na kusaidia wazazi vijana ambao
walikatisha shule kutokana na ujauzito.
Mkurugenzi
huyo pamoja na kueleza changamoto za malezi na ulinzi kwa watoto
amesema sera zilizopo zinaendelea kuboreshwa ili kutoa ulinzi zaidi
katika kuhakikisha taifa linakua na watoto wenye uhakika wa usalama.
Naye
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi
ya watu UNFPA Dk. Natalia Kanem alisema mtoto msichana anahitaji
kushikilia ndoto yake pamoja na changamoto zinazojitokeza.
Alisema
pamoja na kuwepo kwa vikwazo vya mawasiliano , mtoto wa kike anastahili
kupewa taarifa mbalimbali zinazomweka huru katika mambo ambayo
yanamhusu yeye na jamii yake.
Alisema
pamoja na haja ya kuwepo kwa usawa wa kijinsia, mtoto wa kike ni lazima
apate haki yake ya kusoma,kutodhuriwa na utamaduni uliopitwa na wakati
ambao ni kandamizi kama kukeketwa na ndoa za utotoni na kutobaguliwa.
Msaidizi
wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akisoma
risala kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja
vya shule ya msingi Tandale jijini Dar.
Aliwataka watoto wa kike kuhakikisha
kwamba wanasoma kwa kuwa elimu ni kila kitu na wakishakuwa na elimu
watajiamini na kujitambua.
Alisema ipo haja ya kuimarisha mfumo wa
ulinzi kwa watoto wa kike ili kupata nafasi ya kusonga mbele na wale
ambao wamekatishwa masomo kwa sababu mbalimbali kurejea darasani ili
kupata elimu na uwezo wa kuendelea mbele.
Alisema kw akuunganisha nguvu kati ya
serikali, mashirika ya umoja wa mataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo
na mtoto wa kike,watoto wa kike watapata nafasi kubwa ya kusonge mbele.
Aliwataka watoto wa kike kujitambua
kwamba wao ni wazuri lakini wanapaswa kujiheshimu na kuwaheshimu wengine
kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo yao.
“Wale wanaoapata mimba, wale wanaokatishwa masomo ni lazima wapate njia ya kujiendeleza tena” alisema Dk Natalia.
Angel
Benedicto ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani akieleza alipotokea
mpaka kufika alipo sasa wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
yaliyofanyika siku ya Jumamosi.
Katika tamasha hilo wasichana wawili
walitoa ushuhuda, Binti mdogo Eva Tolage ambaye alimwandikia barua Rais
Barak Obama akihoji Marekani na yeye binafsi rais Obama na viongozi wa
dunia watafanya nini kumsaidia mtoto wa kike anayekabiliwa na changamoto
nyingi hasa wale wa vijijini.
Eva alimwambia Barack Obama kwamba
anataka kutimiza ndoto yake ya kuwa askari kusaidia jamii, lakini
atafikiaje ndoto hiyo wakati kuna changamoto ya umeme na huku baba yake
kazi anazofanya hazimpi kipato cha kutosha.
Msichana huyo ambaye aliandika barua kwa
ujasiri mkubwa akihoji maendeleo endelevu yasiyompita binti mdogo
alijibiwa na Rais Obama na kutajwa katika hotuba yake kwenye Umoja wa
Mataifa kwamba viongozi wa dunia akiwemo Barack Obama mwenyewe
wamemsikia na watahakikisha tatizo la wasichana wa Afrika na kwingine
kokote linaondolewa na na wanapata nafasi ya kushiriki katika maendeleo.
Eva
Tolage aliyeandika barua kwa rais Barack Obama wa Marekani na barua
yake kusomwa katika mkutano wa viongozi wa dunia makao makuu ya Umoja wa
Mataifa alitumia mkutano huo kusoma machache aliyoandika. Katika barua
hiyo, Eva mwenye umri wa miaka 15, alielezea jinsi ambavyo bado
mazingira mtoto ni mabovu na hatarishi kiasi cha kumfanya ashindwe
kupata elimu bora, pia kuwa katika hatari ya kukumbwa na vitendo vya
kikatili ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Aidha binti mwingine Angela Benedicto
ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wote sawa alisimulia
matatizo ya wasichana wa kazi,adha zao kutoka kwa wanaume na watoto wa
kiume wanakofanyia kazi.
Alisema kwamba mateso wanayoyapata wasichana wa kazi yanastahili kukoma na kwamba ipo haja ya kuwekwa kwa mfumo unawalinda.
Alisema serikali ina wajibu wa kuwatetea
wasichana kupata haki zao, sio tu kusema shule bure, lakini pia kujenga
kujiamini kwa wasichana katika kutimiza ndoto zao.
Alisema sababu za kuwepo kwa wasichana
wengi wakazi za ndani ni dhuluma inayoambatana na umaskini katika
familia na tamaduni zinazomweka nyuma mtoto wa kike kiasi cha kulazimika
kutafuta kazi za ndani ambazo waajiri wanakuwa hawana staha.
Katika tamasha hilo kulikuwa na shughuli
mbalimbali zikiwemo za kuangalia hali ya afya ya uzazi, elimu ya afya ya
uzazi, kupimwa maambukizi ya UKIMWI na kukaguliwa kwa saratani ya
matiti na kizazi pamoja na elimu yake.
Pia kulikuwa na michezo ya kuigiza na sarakasi na mwanamuziki wa kike mwasiti alichombeza kwa nyimbo zake za uadilifu.
Siku ya Mssichana duniani huadhimkishwa Oktoba 11 lakini kwa Tanzania iliadhimishwa Oktoba 10.
Mgeni
rasmi pamoja na vingozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na
wasichana wenye ulemavu wa ngozi katoka maadhimisho ya siku wa mtoto wa
kike.
Watoto wakiwa na hali ya furaha wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika shule ya msingi Tandale.
Watoto wa kike wakionesha vipaji katika mpira wa miguu wakati wa siku ya mtoto wa kike Duniani.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai (wa kwanza kulia) akivuta kamba pamoja na wanafunzi wa kike huku
Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi.
Hashina Begum (wa kwanza kushoto) akiungana na timu ya wanaume ambapo
timu ya wasichana iliibuka kidedea.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini Mwasiti akitoa burudani wakati wa
maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika katika viwanja vya
shule ya msingi Tandale.
Vijana wa Temeke wakiendelea kutoa burudani.
Wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali wakipatiwa elimu ya afya na uzazi katika mabanda yaliyopo kwenye maadhimisho hayo.
Sehemu ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.
Elimu mbalimbali zikitolewa uwanjani hapo.
Burudani ya nyimbo kutoka kwa wanafunzi.
Wanafunzi wakipitia kumbukumbu mbalimbali kwenye madaftari yao.
Mmoja wa wanafunzi akijibu swali.
Picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale.
Mgeni
rasmi na Mwakilishi wa Shirika la UNFPA pamoja na wadau wanaotetea
masuala ya haki ya mtoto wa kike kwenye picha ya pamoja katika bango
maalum.
Maagizo mbalimbali yanayoonyesha unyanyasaji kwa mtoto wa kike.
Wasanii wakifikisha ujumbe kwa njia ya maigizo.
Umati wa wanafunzi waliohudhuria siku ya mtoto wa kike duniani.
Wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye siku ya mtoto wa kike duniani.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai (kushoto) na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu
duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem ( wa pili kushoto) katika picha ya
pamoja na watoa huduma katika mabanda yaliyokuwepo kwenye maadhimisho
hayo.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem
wakisaini vitabu vya wageni kwenye banda mojawapo walilotembelea.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem
wakipata maeleozo na kukagua shughuli mbalimbali zinazoifanywa na vijana
wa Restless wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai (wa pili kutoka kulia) akipata maelezo kutoka kwa wasichana
wajasiriamali alipokuwa anatembelea mabanda.
Burudani nayo haikuwa mbali katika kusherehesha siku ya mtoto wa kike duniani.
0 comments:
Post a Comment