Monday, 1 December 2014

MAKALA YA UCHUMI: UFUGAJI NYUKI UMEWAKOMBOA WASOMI KIUCHUMI

Wakiwa wanatengeneza mizinga ya kufugia nyuki mkoani Singida

Vijana wa kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha na biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji wa asali na nta


kijana Hamza Rajabu wa kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society ambao ni wahitimu wa vyuo wanaojishughulisha na biashara ya ufagaji nyuki na uuzaji akiwa kwenye maonyesho ya kongamano la ufugaji nyuki lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni 


Na Ferdinand Shayo.Arusha.
Baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu safari inaanza ya kuelekea kwenye jamii na kuanza maisha ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zake ikiwemo suala la ajira ambalo ni suala mtambuka kwa kila mhitimu wa chuo.
Katika harakati za kufanya shughuli za kujiingizia kipato na kutengeneza ajira ,vijana 13 wa mkoa wa Singida ambao wote ni wahitimu kutoka vyuo mbali mbali wanakusanyika na kuanza kufuga nyuki pamoja na kuuza mazao ya nyuki ambayo ni asali,nta na sumu ya nyuki ambayo ni dawa.
Baada ya kuona fursa iliyopo katika sekta ya nyuki wanaamua kuitumia vyema kwa kuanza kufuaga nyuki na kuuza mazao yake ambayo yamewapatia faida za kiuchumi pamoja na kufanikiwa kuuza katika masoko ya nje.
Vijana hao walipohitimu chuo kikuu walijikusanya na kuunda kikundi cha Singida Youth Interprises and consultant cooperative society.
Mmoja wa wanachama wa kikundi hicho ni Hamza Rajabu anaeleza kuwa walianza kufuga nyuki wakiwa wenyewe baadae  wakaungana na vyama vya wafugaji nyuki ambapo tulivuna tani nyingi na kuiuza hadi soko la nje.
Hamza anaeleza kuwa changamoto kubwa iliyokua inawakabili ni ubora wa vifungashio (parking na lebel) lakini waliitatua kwa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu hivyo kufanikiwa.
Kama wahitimu tumefanikiwa kutengeneza vikundi 16 vya wafugaji nyuki na kuwapa ushauri wa kitaalamu,kutengeneza mabanda na vifaa bora vya kuchuja asali.
‘Binafsi nimehitimu chuo cha kilimo SUA mwaka juzi ,tunachokiona hapa kwenye sekta ya nyuki ni wajasiriamali wengi kukosa kuthibitishwa viwangoi na  TBS na  pia kupata vifungashio vizuri.  
Msimu uliopita tulizalisha tani 8 za asali na nta tani 18 kwa Mwekezaji kutoka Marekani .
Wahitimu wao ni kutoka vyuo mbali mbali ikiwemo  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ,St.Agustine University (SUA).
Tunafanya biashara ya kuuza makundi ya nyuki katika sehemu mbali mbali ndani na nje ya Singida ,maeneo ya Nyumba ya nyuki na Iringa.
Wasomi hao wamefanikiwa kutengeneza makundi ya vijana,wazee na kinamama yanayojishughulisha na ufugaji nyuki.
Makundi hayo tunayapa mizinga miwili miwili kama mtaji ambao hutolewa na Mwekezaji kutoka nje kama mkopo wakivuna asali wanamuuzia mwekezaji huyo baada ya miaka miwili wanabaki na mizinga hiyo.
Mizinga inayotolewa ni ile ya kisasa ambayo huuzwa kiasi cha shilingi 65000 huwasaidia wafugaji kutunza asali nyingi ambayo wanaiuza na kuwapatia kipato.
Wakati mwingi tunatoa elimu kwa wafugaji nyuki namana ya kufanya ufugaji wa kisasa na kuvuna asali kwa kuzingatia usafi ,asali ambayo tunaiufungasha na kuiuza ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa wanamiliki mashamba matatu ,moja kwa ajili ya kufuga makundi ya nyuki na kuyauza mengine ni kwa ajili ya asali,nta na sumu ya nyuki.
“Tuna mashamba matatu makubwa tunayatumia katika shughuli ya ufugaji kuku ,mawili yako Kisaki na moja liko wilaya ya Ikundi mkoani Singida.
Tunawashauri Watanzania na wasomi wenzetu wanaohitimu vyuo kutumia fursa lukuki zilizoko katika jamii zao na kujiajiri badala ya kusubiria kuajiriwa.
0765938008

0 comments:

Post a Comment