Monday, 29 December 2014

NASARI AWAPA SOMO WENYEVITI WAPYA WA SERIKALI ZA MITAA KUTUMIKIA WANANCHI IPASAVYO

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari akizungumza na wenyeviti wapya wa mtaa pamoja na wajumbe waliochaguliwa kwa tiketi ya CHADEMA katika Wilaya ya Arumeru Mashariki katika semina iliyoandaliwa na Mbunge huyo ya kuwahamasisha kuwatumikia wananchi ilifanyika katika ukumbi wa usariver academy leo.Picha na Ferdinand Shayo

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari amewataka wenyeviti  wapya wa mitaa waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kutojihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu katika kipindi cha uongozi wao na kusisitiza kuwa chadema sio sehemu ya kupiga dili.

Aidha amewaasa Wenyeviti hao kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya haki kutokana na dhamana kubwa waliyopewa na wananchi  hivyo wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa uongozi na uwajibikaji.

Nassari Akizungumza katika semina ya siku mbili ya Wenyeviti hao na wajumbe yenye lengo la kuhamasisha ufanisi na utendaji kazi wa viongozi hao wapya kabla ya kuingia kazini amesema kuwa wanakwenda kuwatumikia wananchi bila kuwabagua .

“Mmechaguliwa maana yake ni kurudisha tumaini kwa Watanzania ,wananchi waone tofauti  sio tofauti ya kubadilisha bendera na kuweka bendera zenu bali kuwajibika” Alisema Nassari

“Wenyeviti wa mitaa mnapaswa kujua kuwa mbeba dhamana ya watu wengi mikononi mwenu hivyo mnapaswa kuitendea kazi” Nassari

Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Meru Gadieli Mwanda amewataka Wenyeviti hao kujiandaa kufanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi ,utumishi ambao hauko ndani ya CCM.

Katibu wa CHADEMA wilaya Stephano Mungure anaeleza kuwa ushindi walioupata katika vijiji 32 unazidi kukifanya chama hicho kuwa tumaini la wananchi sifa ambayo inatakiwa iendelezwe na viongozi hao.

0 comments:

Post a Comment